IQNA

Al Houthi

Yemen itaendelea kulenga meli zinazohusishwa na Israel katika Bahari ya Sham

11:23 - January 26, 2024
Habari ID: 3478254
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Abdul-Malik al-Houthi anasema kulengwa kwa meli zinazohusishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kutaendelea katika Bahari ya Sham hadi Wapalestina walioko Gaza watakapoweza kupokea misaada.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni siku ya Alhamisi, al-Houthi alisema sababu kuu ya kuendelea jinai za Wazayuni ni msimamo wa Marekani.

Aliongeza kuwa: "Marekani inasisitiza kwamba Gaza ibaki chini ya mzingiro kamili na kivuko cha Rafah kinasalia kufungwa. Marekani inasisitiza kuwa misaada na vifaa vinavyohitajika na watu wa Palestina havitaingia Gaza."

Aidha amesema: "Marekani inatuma maafisa wake katika eneo hilo kusimamia jinai za Wazayuni. Marekani inahusika moja kwa moja katika njaa ya watu wa Palestina. Sio tu kwamba wanawaanzisha, bali wanaipa Israel mabomu ili kuwaua."

Kiongozi wa Ansarullah ameendelea kubainisha kwamba, Marekani sio tu kwamba hairuhusu chakula na dawa kuingia Gaza, lakini pia imezidisha mvutano na Yemen ambao umesababisha hasa kubwa.

Aidha amesema Marekani haijali kuhatarisha meli na kugeuza Bahari ya Sham (Nyekundu) kuwa uwanja wa vita, wala haina tatizo la kupanua wigo wa vita na kushadidisha taharuki hali katika eneo hilo.

Al-Houthi alisema Tangu kuanza kwa operesheni za Yemen katika Bahari ya Sham, meli 4,874 za kibiashara zimepitia Bahari Nyekundu, ambayo ni idadi kubwa.

Kiongozi wa Ansarullah amesisitiza kuwa: "Tunalenga meli za Israeli pekee. Lengo letu ni kutoa shinikizo la kupeleka chakula na dawa kwa watu wa Palestina na kuzuia jinai za Wazayuni."

Waislamu wa Yemen, alisema, wamejionyesha kama mfano katika ngazi zote, akitoa mfano wa maandamano ya kila wiki yanayofanywa kote nchini kupinga mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina.

Kiongozi wa Ansarullah amesema matokeo ya operesheni za Yemen ni kushambulia adui Mzayuni kwa zaidi ya ndege 200 zisizo na rubani na zaidi ya makombora 50 ya balistiki na cruise.

4195913

Al-Houthi alisema wananchi katika nchi ambazo tawala zinawakandamiza vikali na hivyo hawawezi kushiriki maandamano wanaweza kuunga mkono Palestina kwa kususia bidhaa za Marekani na Israel.

Aidha amesema Waislamu wana jukumu kubwa la kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Akifafanua amesema lau Waislamu wangetoa msaada unaohitajika kwa watu wa Palestina na wapiganaji wa Kiislamu, mlingano huo ungebadilika kabisa.

Al-Houthi alisema licha ya msaada wa kifedha na kijeshi wa Marekani na Magharibi, hasara ya kijeshi na kiuchumi ya Israel kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni kubwa.

captcha