IQNA

Al-Masjid An-Nabawī

Msikiti wa Mtume SAW wakaribisha waumini milioni 5.9 kwa wiki

11:30 - April 26, 2024
Habari ID: 3478735
IQNA - Mamlaka za Saudia zimeripoti kuwa zaidi ya waumini milioni 5.9 walitembelea Msikiti wa Mtume (Al-Masjid An-Nabawī) wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Utunzaji wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume, watu 598,939 walitembelea kaburi la Mtume Muhammad (SAW), na waumini 254,209 waliswali katika Al-Rawdah Al-Sharifa.

Ripoti hiyo pia ilionyesha kuwa wazee 9,172 na watu wenye ulemavu walipata huduma maalumu za kuwasaidia kuzuru eneo hilo takatifu..

Mamlaka hiyo ilibainisha kuwa wageni 22,627 walinufaika na huduma za mwongozo, 157,464 walipata huduma za wakalimani, na 12,884 walifika kwenye maktaba ya Msikiti wa Mtume.

Jumla ya zawadi 153,068 zilisambazwa kwa wageni, na watu 61,207 walitumia huduma za usafirishaji.

Ripoti hiyo pia ilitaja usambazaji wa chupa 180,880 za maji ya Zamzam na milo ya Iftar 226,193 katika korido za msikiti zilizotayarishwa kwa ajili ya wanaofunga.

Kishikizo: al masjid an nabawi
captcha