IQNA – Magaidi walifyatua risasi ndani ya msikiti katika eneo la kaskazini-kati mwa Nigeria wakati wa Swala ya Alfajiri siku ya Jumanne, na kuua angalau watu 27, maafisa wa eneo hilo na wakazi wamesema.
IQNA – Wosia wa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) kuhusu Ahlul-Bayt (AS), Qur’an Tukufu, na ulazima wa kulinda umoja wa Waislamu unaonyesha dira yake ya kujenga jamii yenye mshikamano na haki, amesema msomi mmoja.
IQNA – Zaidi ya watoto 3,000 wamekusanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) mjini Mashhad kwa ajili ya kongamano la Qur’ani lililopewa jina “Malaika wa Muqawama (Upinzani)”, na kujaza eneo hilo tukufu kwa tilawa na sauti za imani.
IQNA – Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu ya Mfalme Abdulaziz yanatarajiwa kufikia tamati kwa hafla maalum itakayofanyika mjini Makkah siku ya Jumatano.
QNA – Msafara wa Qur’ani wa Arbaeen kutoka Iran, unaojulikana mwaka huu kama “Msafara wa Imam Ridha (AS)”, ulianza shughuli zake katika njia ya Arbaeen tarehe 8 Agosti 2025.
IQNA – Washiriki wa Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mfalme Abdulaziz wametembelea misikiti ya kihistoria na maeneo ya turathi katika mji wa Madina, kama sehemu ya programu ya kitamaduni iliyoandaliwa na mamlaka za Saudi Arabia.
IQNA – Fathima Sajla Ismail kutoka jimbo la Karnataka, India, amekamilisha kuandika Qur’ani Tukufu yote kwa mkono akitumia kalamu ya jadi ya kuzamisha kwenye wino (dip pen).
IQNA – Jumapili, mji wa Banihal katika eneo la Kashmir linalosimamiwa na India uliandaa Mkutano wa Pili wa Qur’ani ya Braille kwa watu wenye ulemavu wa kuona.
IQNA – Gavana wa mkoa wa Kafr el-Sheikh nchini Misri amesema kuwa marehemu qari Sheikh Abulainain Shuaisha alikuwa balozi bora wa Qur’ani na ataendelea kubaki kuwa fahari ya Misri.
IQNA – Mchujo wa awali wa usomaji kwa ajili ya Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu umekamilika, ambapo kazi kutoka nchi 36 zimepitiwa.
IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Kiirani amehimiza ushirikiano imara kati ya misikiti duniani, akisisitiza haja ya hatua za pamoja kulinda Msikiti wa Al-Aqsa dhidi ya uvamizi unaendelea wa utawala ghasibu wa Israel.
IQNA – Mwanazuoni wa dini kutoka Qom amemwelezea Mtume Muhammad (SAW) kuwa ndiye kielelezo bora kabisa kwa wanadamu, akisisitiza kuwa tabia yake njema ni mwongozo wa kudumu kwa Waislamu wa leo.
IQNA – Awamu ya awali ya kategoria ya usomaji katika Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi Waislamuyaliyoandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza rasmi, huku washiriki kutoka mataifa 36 wakituma video za usomaji kwa ajili ya tathmini.
IQNA – Muhammad Hussein al-Tayyan, mwandishi na mtaalamu wa lugha wa Syria, anaamini kwamba Qur’an ni kitovu cha lugha ya Kiarabu, na kupitia Qur’an ndiyo lugha hii iliyoenea na kukomaa.