IQNA

Waislamu Ulaya

Mwigizaji Donnie Roelvink atangaza Kusilimu

9:58 - April 22, 2024
Habari ID: 3478714
IQNA - Mwigizaji wa Uholanzi Donnie Roelvink amesilimu siku ya Ijumaa, Aprili 19, kwa kutamka Shahadah.

Donny anayejulikana pia kama mwenye ushawishi katika mitandao ya kijamii,  alionekana kwenye video ya mtandaoni kwenye Instagram akitakmka shahada ndani ya msikiti.

"Sidhani kama watu wengi wamegundua kuwa nilikuwa na siku maalum jana," Roelvink alisema katika ujumbe wake wa video kwenye Instagram, Telegraaf iliripoti.

"Picha zilichukuliwa, kuwekwa mtandaoni na kuripotiwa sana kwenye vyombo vya habari. Hilo lilitarajiwa nikifanya hivyo mbele ya kundi kubwa la watu.”

Mnamo 2022, Donny, 26,  alijeruhiwa wakati akipiga video ya mazoezi ya mwili na marafiki. Aliishia hospitalini akiwa amevunjika mbavu tano na majeruhi kwenye mapafu yake yameanguka. Alichukua wiki kadhaa kabla hajapona.

Mwaka huo huo, aliambiwa ana saratani ya tezi dume. Kwa sababu ya matukio hayo mawili, alianza kuimarisha imani yake, hatimaye akaamua kufuata Uislamu maishani.

Katika wiki zilizopita, Donny amekuwa akitembelea msikiti huo, alifungwa mwezi wa  Ramadhani, na amekuwa akisoma Qur'ani tukufu kwa muda.

Uislamu ndio dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani, huku idadi ya Waislamu ikitarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya mara mbili duniani kote kati ya 2015 na 2060 kulingana na utafiti wa Kituo cha Utafiti cha Pew.

Mwaka jana, Rodtang Jitmuangnon, bingwa wa ONE Championship uzito wa flyweight Muay Thai, alisilimu.

Mwanasoka wa Ujerumani Robert Bauer amesilimu na kuwa Muislamu, na kutangaza uamuzi huo kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram.

3488026

Kishikizo: kusilimu uholanzi
captcha