IQNA

Mcheza Soka maarufu wa Uholanzi, Seedorf , atangaza kuwa amesilimu

11:41 - March 06, 2022
Habari ID: 3475015
TEHRAN (IQNA) – Kiungo wa kati wa zamani wa Timu ya Soka ya Uholanzi Clarence Seedorf ameikumbatia dini tukufu ya Kiislamu.

Seedorf ambaye pia aliwahi kuwa kiungo wa zamani wa AC Milan, Real Madrid na Ajax alitoa tangazo hilo kupitia ukurasa wae Instagram, akisema: "Shukrani za kipekee kwa jumbe zote nzuri za kusherehekea kujiunga na familia ya Kiislamu."

"Nina furaha na nimefurahi kujumuika na Ndugu na Dada wote duniani hasa [mke wangu] Sophia [Makramati] ambaye amenifunza kwa undani zaidi maana ya Uislamu.

"Sikubadilisha jina langu na nitaendelea kubeba jina langu kama nilivyopewa na wazazi wangu, Clarence Seedorf! Ninatuma upendo wangu wote kwa kila mtu ulimwenguni."

Akichukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji waliofanikiwa zaidi katika historia ya Kombe la Mabingwa Ulaya, UEFA, Seedorf ndiye mwanasoka pekee aliyeshinda Kombe la UEFA akiwa na vilabu vitatu tofauti.

Kiungo huyo ambaye anazungumza angalau lugha sita - alicheza katika timu ya taifa ya Uholanzi mara 87 na alicheza katika Mashindano matatu ya UEFA ya Soka ya Ulaya na Kombe la Dunia la FIFA la 1998, na kutinga nusu fainali ya mashindano matatu ya mwisho.

Baada ya kustaafu kutoka uwanjani, aliendelea kuwa meneja wa timu kadhaa zikiwemo AC Milan na timu ya taifa ya Cameroon.

Mwaka jana, Seedorf alijiunga na bingwa wa zamani wa UFC Khabib Nurmagomedov, mmoja wa wanariadha mashuhuri wa Kiislamu katika miongo ya hivi karibuni, kuzindua Klabu ya Utendaji ya Seedorf Khabib, chuo cha soka ambacho walisema kitatumia "mbinu ya kipekee ya mafunzo" ambayo inachanganya mpira wa miguu na sanaa za mapigano kama vile karate.

"Tuna misheni sawa maishani," Seedorf alisema. "Tunataka kurudisha kitu kwa vizazi vichanga."

"Tutaleta ujuzi, makocha na mbinu, ufuatiliaji na usaidizi kutoka kwa mtazamo wa masoko ili kusaidia ukuaji wa kila ukumbi na kila ushirikiano."

3478049

captcha