IQNA

Kuarifisha Uislamu

Wasio Waislamu watembelea Msikiti wa Fatih Amsterdam kujifunza kuhusu Uislamu

15:49 - November 07, 2022
Habari ID: 3476051
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya watu 1,000 wasio Waislamu walitembelea Msikiti wa Fatih huko Amsterdam, Uholanzi, baada ya msikiti huo kuwafungulia milango wafuasi wa imani nyingine.

Wageni waliotembelea msikiti huo, ambao unafungamana na Idara ya Kidini ya Uturuki- Diyanet- (TDV), walipata taarifa kuhusu Uislamu, misikiti na sanaa za Kiislamu.

"Waholanzi wana hamu sana kuhusu dini ya Uislamu na muundo wa ndani wa msikiti wetu," alisema Kemal Gözütok wa Msikiti wa Fatih. "Wanataka kujifunza kila kitu kuanzia kabati la viatu hadi minbar, kutoka mihrab hadi vigae."

Jengo la Msikiti wa Fatih lilibadilishwa kutoka kanisa ambalo halikuwa na wafuasi tena na kuwa msikiti mnamo 1981 na liliunganishwa na Wakfu wa Kidini wa Uholanzi mnamo 1986.

Mgeni mmoja aliyejitaja kwa jina la Charn kutoka Marekani, alisema ingawa aliishi karibu sana na msikiti huo ilikuwa ni mara ya kwanza kuingia ndani: "Nilipenda sana mambo ya ndani ya msikiti. Sauti za maimamu zilikuwa zilikuwa na mvuto."

Mgeni mwingine, Jaap Kapteyn, alitaja umuhimu wa kutembelea msikiti na kuutangaza Uislamu kupitia shughuli za sanaa . "Ni njia nzuri sana ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi," alisema.

3481152

Kishikizo: uholanzi waislamu
captcha