IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Chuki dhidi ya Uislamu imeenea katika taasisi zote za serikali nchini Uholanzi

20:36 - September 23, 2023
Habari ID: 3477642
AMSTERDAM (IQNA) –Rais wa taasisi kuu ya Kiislamu Uholanzi anasema chuki dhidi ya Uislamu inaweza kuonekana katika taasisi zote za serikali nchini humo.

Muhsin Koktas, mkuu wa Shirika la Mawasiliano ya Waislamu na Serikali (CMO) nchini Uholanzi amesema hakushangazwa na uchunguzi wa siri kuhusu Waislamu na taasisi za Kiislamu nchini Uholanzi, baada ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi nchini Uholanzi na Ulaya baada ya 2010.

Koktas alisema si bure kwamba hali ya Waislamu kutokuwa na imani kwa serikali imekuwa ikiongezeka hivi karibuni, na inaonekana kwamba serikali pia haina imani na Waislamu, na ndiyo maana walifanya uchunguzi huu".

Akieleza kuwa chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi inaweza kuonekana katika taasisi zote za serikali, Koktas alisema: "Wakati Wizara ya Masuala ya Kijamii na Ajira inashughulikia kurejesha imani ya Waislamu na kufanya majadiliano, kwa upande mwingine, Waziri wa Sheria na Usalama, Dilan Yesilgoz, anasema hakuna nafasi ya hijabu katika sare za polisi na hivyo amepiga marufuku vazi hilo.Matukio ya ubaguzi wa rangi katika Wizara ya Mambo ya Nje NA  kashfa ya ubaguzi katika ofisi ya ushuru  baadhi tu ya matukio ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi katika taasisi nyingi za serikali. "

Koktas alisema kutokana na ubaguzi wa rangi na ubaguzi katika taasisi za serikali, imani ya Waislamu kwa serikali imeshuka kwa kiasi kikubwa.

Mnamo 2021, ilifichuliwa kuwa nchini Uholanzi manispaa zilifanya uchunguzi wa siri katika misikiti na taasisi zinazomilikiwa na Waislamu kupitia kampuni za kibinafsi.

Iliripotiwa kuwa utafiti uliofadhiliwa na Shirika la Usalama na Kupambana na Ugaidi la Uholanzi (NCTV) ulifanywa kupitia kampuni binafsi ya NTA (Nuance door Training and Advies).

Ilisema wafanyakazi wa NTA wanaofanya utafiti misikitini walijitambulisha kuwa ni Waislamu wanaosali jamaa mara kwa mara au wasafiri kutoka nchi za kigani, na wakati wa uchunguzi huo, walikutana na waumini wanaosalia misikitikini bila kufichua utambulisho wao.

Karien van Gennip, Waziri wa Masuala ya Kijamii na Ajira, alisema katika barua yake kwa Baraza la Wawakilishi wiki hii kwamba imebainishwa kuwa wakala huo ulifanya utafiti usioidhinishwa kuhusu watu binafsi, taasisi na mitandao miongoni mwa jamii za Kiislamu.

Van Gennip alielezea masikitiko yake kuhusu uchunguzi wa siri wa Waislamu na taasisi za Kiislamu na akasema amepata funzo kwa ajili ya siku zijazo.

3485284

captcha