IQNA

Msikiti wahujumiwa nchini Uholanzi

15:12 - December 17, 2020
Habari ID: 3473466
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mmoja umehujumiwa katika mji wa Amsterdam nchini Uholanzi. Kwa mujibu wa taarifa gaidi aliyekuwa amevaa barakoa aliurushia mawe Msikiti wa Hagia Sophia mjini Amsterdam.

Hatahivyo mbali na madirisha kuvunjwa hakuna hasara iliyopatikana katika hujuma hiyo.

Wasimamizi wa msikiti huo wamesema watawasilisha lalalmiko ramsi dhidi ya aliyetekeelza hujuma hiyo inagawa utambulisho wake haujaweza kubainika.

Waislamu nchini Uholanzi wameingiwa na wasi wasi kutokana na misikiti kulengwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu katika miezi ya hivi karibuni na wametaka polisi nchini humo kuhakikisha maeneo ya ibada ni salama.

Hivi karibuni pia Msikiti wa Jamia wa Utrecht nchini Uholanzi ulishambuliwa na watu wasiojulikana.

Mashambulizi kama hayo yamepelekea wasio wasio kuongezeka miongoni mwa Waislamu.

3941415

captcha