IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wawakilishi wa nchi 30 wanashiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an ya Rwanda

15:39 - April 21, 2024
Habari ID: 3478709
IQNA - Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yanafanyika nchini Rwanda leo Jumapili.

Wajumbe kutoka zaidi ya nchi 30 za Afrika wamewasili katika mji mkuu wa Rwanda Kigali kabla ya mashindano hayo.

Hafal hiyo ya kimataifa ya Qur'ani inafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Wilaya ya Gicumbi, na Kambi ya Kigali mnamo Aprili 21.

Mashindano ya kuhifadhi  Qur'an yanachukuliwa kuwa muhimu katika kutangaza ujumbe wa amani kwa wote kupitia Quran, na pia yanalenga kuhifadhi utamaduni na mila za Kiislamu.

Mashindano haya yanaunganisha wasomi, wahubiri, na wasomaji wa Qur'ani kutoka kote ulimwenguni.

Wakati huo huo, washindi wa shindano hilo watapokea mbalimbali za fedha na pia kupewa vyeti.

Waandalizi wanasema tuzo hiyo inawapa motisha vijana  kushikamana na dini yao na kutimiza wajibu wao kwa Uislamu ambao msingi wake ni amali njema, uvumilivu na mshikamano.

3488016

captcha