IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

Wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi 9 katika Jopo la Majaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran

16:11 - February 15, 2024
Habari ID: 3478354
IQNA - Jopo la majaji wa Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linajumuisha wataalamu wa Qur'ani kutoka taifa mwenyeji pamoja na nchi nyingine nane.

Duru ya mwisho ya mashindano hayo inatazamiwa kuanza katika sherehe mjini Tehran leo jioni.
Katika toleo hili la mashindano hayo, wataalamu wa fani tofauti za Qur'ani kutoka Iran, Kuwait, Syria, Bahrain, Iraq, Indonesia, Lebanon, Afghanistan, na Bangladesh watawatathmini  washindani.

Hii hapa orodha ya jopo la waamuzi katika sehemu ya wanaume:
Tajweed: Abbas al-Balushi kutoka Kuwait na Heidar Kasmaei na Masoud Sayyah Gorji kutoka Iran.
Lahn: Imad Rami kutoka Syria na Mahmoud Lotfinia na Hassan Mokhtari kutoka Iran
Sawt: Ahmed bin Yusuf al-Azhari kutoka Bangladesh na Muhammad Abbasi na Nosratollah Hosseini kutoka Iran.
Waqfu na Ibtida: Khairuddin al-Hadi kutoka Iraq na Karim Dolati na Hassan Hakimbashi kutoka Iran.
Kukariri Kuhifadhi Qur'ani: Zia al-Haq Minqad kutoka Afghanistan na Mohammad Sadeq Nasrollahi na Mehdi Abbasi kutoka Iran.
Katika sehemu ya wanawake, Bi. Mahboubeh Kateb anaongoza jopo hilo, ambalo pia linajumuisha Fatimah Kazu kutoka Syria, Fatimah Alwash kutoka Lebanon, Maria Alfa kutoka Indonesia, Mahi Kamaleddin kutoka Iraq, Zaynab al-Makhlouq kutoka Bahrain na Marjaleh Niavarani, Sediqeh Barani, Parisa Mojarad, Seyedeh Fatemeh Mirghiyasi, na Fatemeh Mandegarmehr kutoka Iran.
Wahifadhi na wasomaji Qur'ani kutoka nchi 110 walijiandikisha kwa ajili ya mashindano hayo mwaka huu na baada ya duru ya awali, washiriki 69 kutoka nchi 40 wamefanikiwa kuingia fainali.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni hafla ya kila mwaka inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, ambayo huwavutia wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
 4199898

Habari zinazohusiana
captcha