IQNA

Harakati za Qur'ani

Nchi 40 Zahudhuria Mashindano ya Kimataifa ya Qur’an ya Algeria

19:03 - February 05, 2024
Habari ID: 3478307
IQNA - Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 40 wanashiriki katika mashindano ya 19 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Algeria.

Haya ni kwa mujibu wa Youcef Belmehdi, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini wa Algeria, akizungumza katika kongamano katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Algiers.

Duru ya awali ya mashindano hayo ilianza Jumapili katika kategoria za kuhifadhi na usomaji wa Qur'ani Tukufu.

Tuzo hilo lililopewa jina la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Algeria, huandaliwa kila mwaka chini ya usimamizi wa rais wa nchi hiyo.

Washindi watatajwa na kuheshimiwa katika sherehe iliyopangwa kufanyika kwa mnasaba wa Isra na Miraj au Mab'ath ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Kwingineko katika matamshi yake kwenye kongamano hilo, Belmehdi alisifu juhudi za shughuli za Qur'ani za Algeria na shakhsia wa Qur'ani katika kuhudumia Kitabu Kitukufu.

Vile vile amebainisha kuwa maelfu ya watu kutoka baadhi ya nchi 90 wamejiandikisha kwa ajili ya kozi za Qur'ani Tukufu za mtandaoni zinazoandaliwa na Algeria, akisema hilo linaonyesha umuhimu ambao serikali za Algiers inatilia maanani elimu ya Qur'ani.

Miaka michache iliyopita wakati wa kuenea kwa janga la coronavirus, Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kidini ya Algeria iliandaa kozi za mtandaoni za kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kozi hizo zimekuwa zikifanyika kila mwaka tangu wakati huo.

Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

3487084

Habari zinazohusiana
Kishikizo: algeria qurani tukufu
captcha