IQNA

Afya ya Akili Katika Qur'ani /2

Kumkumbuka Mungu ni Sharti la Afya ya Akili

20:12 - January 24, 2024
Habari ID: 3478247
IQNA - Moja ya dhana muhimu katika afya ya akili ni amani ya akili, ambayo inaweza kupatikana wakati moyo na ulimi wa mtu hujazwa na kumbkumbuka au kumtaja Mwenyezi Mungu.

 

Hali inakuja wakati dhikri au kumkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu hukithir katika mawazo ya mtu, hisia na tabia.

Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 28 ya Surah Ar-Ra’ad: “Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!”

Kwa mtazamo wa Uislamu, hadhi ya juu zaidi ya mwanadamu hupatikana wakati mtu anapokuwa katika hali ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu na hapo nuru ya Mwenyezi Mungu inamulika moyoni mwake. Ni katika hali hiyo ndipo akili ya mtu hufikia amani na utulivu.

Mwenyezi Mungu anasema katika Quran: “Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisio mkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri." . (Aya ya 22 ya Surah Az-Zumar)

Ndio maana inapotokea msiba au dhiki watu wanashauriwa kusema, “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye hakika tutarejea. (Aya ya 156 ya Surah Al-Baqarah)

Kwa hiyo hatua moja muhimu kuelekea kupata afya ya akili, kuponya masuala ya kiakili na matatizo, na kufikia amani ya akili na uhakika ni kumkumbuka Mungu.

Pia, Dhikr  ni njia ya kuponya uzembe na kusonga mbele kwenye njia ya kukua na kuchipuka kwa uwezo wa kibinadamu. Kwa hiyo, ili kupata amani maishani, tunapaswa kumkumbuka Mwenyez Mungu, kumuomba na kukimbilia kwake. Sala ya kila siku yenyewe hujenga amani ya akili kwa sababu kuomba ni miongoni mwa mifano ya kumkumbuka Mwenyezi  Mungu.

Katika Aya ya 83-84 ya Surah Al-Anbiya, Mwenyezi Mungu anarejea kwenye kisa cha Nabii Ayubu (AS) na kusema, “Na Ayubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu. Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada."

3486928

Kishikizo: qurani tukufu Afya
captcha