Hili ni muhimu ili kuepusha mzozo wowote wa kidini katika siku zijazo, Mwakilishi Maalum wa Waziri Mkuu wa Pakistan kuhusu Maelewano ya Dini Mbalimbali na Mashariki ya Kati Hafiz Muhammad Tahir Mehmood Ashrafi alisema huko Lahore Jumapili.
Akilaani kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi chini ya mwamvuli rasmi, alisema kuwa wahusika wa matukio hayo wanataka kuleta mgongano kati ya mataifa na dini.
Ashrafi, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Pakistan, aidha alisema kuwa magaidi waliowaua watu bila ya sababu yoyote kwa jina la Uislamu hata hawakuwa Waislamu. Alisema Waislamu wanawaheshimu manabii wote watakatifu na vitabu vya Mwenyezi vikiwemo Biblia, Taurati na Zaburi kwani ni sehemu ya imani ya Waislamu
Alisema kuwa ni ishara nzuri kwamba dini zote zikiwemo za Kikristo, Kihindu na Sikh zililaani kuchomwa moto kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na takriban nchi zote kubwa pia zimelaani tukio hilo.
3484281