IQNA

Kadhia ya Kashmir

Pakistan yalaani Juhudi za India kuonyesha Mapambano ya Uhuru huko Kashmir kama Ugaidi

19:58 - August 19, 2022
Habari ID: 3475646
TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia mwandamizi wa Pakistan amekashifu juhudi za India za kuonyesha haki halali ya mapambano ya uhuru wa Kashmir kama aina ya ugaidi.

Pakistan imeliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba India ilikuwa inakandamiza mapambano ya watu wa Kashmir kudai uhuru, kwani hakuna juhudi zozote zilizofanywa kutofautisha ugaidi na harakati za kutafuta haki halali ya watu kujitawala na ukombozi wa taifa.

"Haki hii (ya kujitawala) ni ya asili na iliahidiwa kwa watu wa Kashmir na Baraza la Usalama," Balozi Munir Akram alisema katika majibu ya maandishi kwa hotuba iliyotolewa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa India mnamo Agosti 9 wakati wa kikao cha baraza la usalama kuhusu, "Vitisho kwa Amani na Usalama wa Kimataifa vinavyosababishwa na vitendo vya kigaidi."

Ruchira Kamboj, mjumbe wa India, alikariri madai ya mara kwa mara kwamba Pakistan - bila kutaja jina - ilikuwa inasaidia baadhi ya vikundi vya kigaidi, na pia alielezea kushangazwa kwamba ripoti ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na ugaidi haizingatii shughuli za makundi kadhaa yaliyopigwa marufuku hasa yale ambayo alisema yanalenga India mara kwa mara.

Akikanusha madai ya India,  Balozi Akram alikariri kuwa serikali yake  inalaani vikali ugaidi katika "aina zake zote ", akisema kwamba Pakistan ilikuwa mwathirika mkuu wa ugaidi na iliendelea kuteseka na mashambulio kutoka kwa vikundi vya kigaidi vinavyohusishwa na ISIS kama vile TTP (Tehreek-e -Taliban Pakistan) na JuA (Jamaat-ul-Ahrar) zinazotoka nje ya mipaka ya Pakistan,  na ambavyo "mara nyingi hufadhiliwa na kuungwa mkono kifedha na adui wetu wa eneo."

3480153

captcha