IQNA

Jinai za Israel

Umoja wa Mataifa watakiwa ushinikize Israel isitishe mauaji ya Wapalestina wasio na hatia

12:34 - July 14, 2022
Habari ID: 3475503
TEHRAN (IQNA) – Kundi moja la kutetea haki za binadamu limeutaka Umoja wa Mataifa kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe sera za kutumia mabavu ambayo hupelekea idadi kubwa ya Wapalestina kupoteza maisha.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Med Monitor limemtumia barua Morris Tidball-Binz, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji nje ya mkondo wa sheria au mauaji ya kiholele  na kusema, "Maagizo rasmi yaliyopokelewa na jeshi la Israel katika kukabiliana na raia wa Palestina yalisababisha matumizi ya kimfumo ya nguvu zinazosababisha mauaji, na hivyo kusababisha ongezeko kubwa la matukio ya mauaji ya kiholela katika maeneo ya Palestina," ilisema katika barua iliyotumwa kwa.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, jeshi la utawala haramu wa  Israel limewaua karibu Wapalestina 53 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na al-Quds (Jerusalem) Mashariki, kutokana na sera ya utumiaji nguvu kupita kiasi dhidi ya Wapalestina, barua hiyo ilisema.

Wanajeshi wa Israel wanatumia nguvu kuua kimakusudi Wapalestina, barua hiyo iliongeza, ikinukuu mauaji ya Rafiq Riyad Ghannam huko Jenin wiki iliyopita.

Jumatano iliyopita, vikosi vya Israel vilivamia mashariki mwa mji wa Jaba' huko Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, na kuvamia nyumba moja na kumuua Ghannam, 21, ambaye alitoka nje ya nyumba yake akiwa amevalia nguo za kulalia baada ya kusikia sauti isiyo ya kawaida nje.

Tukio hilo la ufyatuaji risasi linaonyesha sera ya Israeli ya kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wasio na silaha ambao, mara nyingi, sio hatari inayotaka matumizi ya risasi, ilisema barua hiyo.

"Tukio hilo linaakisi amri rasmi ya Israel iliyotolewa kwa jeshi ya kutaka raia Wapalestina wafyatuliwe risasi hata kama  hakuna dharura," kundi hilo la haki za binadamu liliongeza.

Kulingana na kundi hilo  la haki za binadamu, sera ya jeshi la Israel ya kufyatua risasi ilikuwa tayari ilikuwa dhaifu huko nyuma na mara nyingi ilisababisha mauaji ya kiholela bila uhalali; hata hivyo, kupitishwa kwa sera mpya ya ufyatuaji risasi mapema mwaka 2021, kuliifanya kuwa mbaya zaidi ambapo  wanajeshi wa utawala hatili wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wamepata idhini rasmi ya kuwafyatulia risasi Wapalestina waliokuwa wakirusha mawe.

Barua hiyo ilisema kuwa maagizo hayo mapya yalifanya kufyatua risasi kuwa jambo rahisi kwa askari hao, hasa kwa uwepo dhamana rasmi ya kuwalinda dhidi ya uwajibikaji wowote.

"Kutokuwepo kwa uwajibikaji ndani ya Israel na jumuiya ya kimataifa kuendelea kunyamazia kimya jinai za Israel zilizofanyika siku za nyuma" kumewezesha vikosi vya Israel kutumia mabavu ya kiwango cha juu dhidi ya raia.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu  limeuhimiza Umoja wa Mataifa kuishinikiza Israel kutii azimio la umoja huo kuhusu "kuzuia mauaji ya kiholela na kucunguza mauaji ya kiholela yanapotokea."

Barua hiyo ilimtaka Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa na vyombo vingine vinavyohusika kufuatilia na kuchunguza mauaji ya raia wa Palestina, kuwalinda na kuchukua hatua za dhati kuhakikisha uwajibikaji kwa mauaji ya kiholela.

3479698

captcha