IQNA

Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yaanza

21:04 - March 01, 2022
Habari ID: 3474992
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran imeanza mjini Tehran siku ya Jumatatu usiku.

Sherehe za kuanza fainali za mashindano hayo zimehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwemo Mwenyekiti wa Shirika la Wakfu na Masuala ya Kheri Iran Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyed Mehdi Khamoushi.

Jumla ya washiriki 62 kutoka nchi 29 wanashiriki katika mashindano kwa njia ya intaneti na baadhi kwa kuhudhuria ana kwa ana ambapo wanashindana katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.

Akihutubu katika sherehe hiyo, Hujjatul Islam Khamousi amesema nara na kaulimbiu ya mashindano ya mwaka ni "Kitabu Kimoja Umma Mmoja." Amesema mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran ni kati ya mashindano makongwe zaidi duniani ya aina yake.

Ameongeza kuwa, mashindano hayo yanalenga kuarifisha Qur’ani Tukufu kama kitabu cha fikra na maisha, sambamba na kuwaenzi wasomaji na waliohifadhi Qur’ani Tukufu na wakati huo huo kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu duniani.

Hujjatul Islam Khamoushi amesema kufanyika mashindano hayo pamoja na kuwepo janga la corona ni ishara kuwepo hai Uislamu na Qur’ani Tukufu. Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma imara ya kustawisha utamaduni wa Qur’ani kote duniani.

Sambamba na mashindano ya 38 ya kimataifa ya Qur'ani tukufu, yatafanyika pia mashindano ya saba ya Qur'ani kwa wanafunzi wa skuli za nchi za Ulimwengu wa Kiislamu na vilevile mashindano ya tano ya Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu kwa washiriki wenye ulemavu wa macho.

Wawakilishi wa Tanzania, Kenya, Uganda ni miongoni mwa walioingia fainali za mashindano ya Qur'ani mwaka huu nchini Iran.

Head of the Awqaf and Charity Affairs Organization Hojat-ol-Islam Seyed Mehdi Khamoushi

Opening ceremony of Quran Competitions in Tehran

4039578

captcha