IQNA

Mchoro wa Shahidi Soleimani wapandishwa Beirut

22:40 - December 26, 2021
Habari ID: 3474725
TEHRAN (IQNA)- Ikiwa imesalia siku chache kabla ya kumbukumbu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Solemani, mchoro mkubwa wa kamanda huyo na wanajihadi wenzake waliouawa shahidi umepandisha katika barabara kuu inayolekea uwanja wa ndege wa Beirut nchini Lebanon.

Mchoro huo una picha za Shahidi Soleimani, Shahidi Abu Mahdi Muhandis na wanajihadi wengine waliokuwa nao ambao pia waliawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani Januari 2020.

Mchoro huo una nara isemayo “Nahnu Qassem” yaani “Sisi ni Qassem”

Aidha watu wa Lebanon wanapanda miche 12,000 kote katika nchi hiyo kumkumbuka Shahidi Soleimani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
Houri ambaye ni mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Algeria ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kupambana na maadui wa Umma wa Kiislamu na kuunga mkono ukombozi wa Palestina na Quds Tukufu. Amesema ni lazima Marekani ijibu mashtaka ya kuhusika na mauaji ya kamanda huyo Muirani kwani kitendo hicho likuwa ni jinai ya kivita.

Katika kutekeleza ahadi yake ya kulipiza kisasi kikali kwa Marekani kutokana na nchi hiyo kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na shakhsia wengine aliokuwa nao, Iran ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya askari gaidi wa Marekani ya Ain Assad nchini Iraq.

4023678

captcha