Taarifa zinasema ugonjwa wa corona unaenea zaidi katika makazi yenye msongamano mkubwa katika mitaa ya mabanda na kambi za vibarua wa kigeni.
Hadi kufikia Jumatatu, mji wa Makka wenye idadi ya watu milioni mbili, ulikuwa na watu 1,050 walioambukizwa corona ikilinganishwa na mji mkuu wa Saudia Riyadh ambao wakati huo ulikuwa na wagonjwa 1,422 pamoja na kuwa ni mkubwa mara tatu zaidi ya Makka.
Idadi kubwa ya raia wa kigeni ambao hawajasajilia na pia msongamano mkubwa katika kambi za vibarua wa kigeni ni mambo ambayo yamefanya iwe vigumu kudhibiti kuenea corona njini humo.
Mwezi Machi, wafanyakazi watano wa Shirika la Binladin, ambalo ni shirika kubwa zaidi la ujenzi Saudia, walippatikana na ugonjwa wa corona. Hali hiyo ilipelekea wakuu wa Saudia waweke karantini katika kambi ya wafanyakazi 8,000 wa shirika hilo na kusitisha kwa muda kazi za upanuzi wa Msikiti Mtakatifu wa Makka.
Kuhakikisha kuwa ugonjwa wa corona hauenei katika mji wa Makka ni muhimu kwa itibari ya ufalme wa Saudi Arabia ambao watawala wake wanajinadi kuwa ni wahudumu wa misikiti miwili mitakatifu ya Kiislamu katika miji ya Makka na Madina.
Hadi kufikia Aprili 14, watu 5,369 walikuwa wameabukizwa corona Saudia na 73 wameaga dunia huku kukiwa na ripoti kuwa ufalme huo unaficha idadi halisi ya walioambukizwa na kufariki kutokana na ugonjwa huo hatari.