IQNA

Mashindano ya Qur'ani Ulaya kufanyika nchini Sweden

12:26 - July 12, 2017
Habari ID: 3471062
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya Qur'ani Tukufu barani Ulaya yamepwanga kufanyika katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatafanyika katika Kituo cha Kiislamu Cha Imam Ali AS mjini Stokcholm kuanzia Septemba 8.

Afisa wa kituo hicho Aqil Zahiri amesema mashindano hayo yatafanyika chini ya uratibu wa Baraza la Mashindano ya Qur'ani la Ulaya Kaskazini, na kwamba mwaka huu, kutokana na maombi ya wasomaji wa nchi zingine za Ulaya, mashindano ya mwaka huu hayatajumuisha tu washiriki wa kaskaizni mwa bara hilo bali maeneo yote ya Ulaya. Aidha amesema mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur'ani, Adhana na ufahamu wa Qur'ani Tukufu.

Zahiri amesema mashindano hayo yanalenga kustawisha utamaduni na mafundisho ya Qur'ani, umoja wa Waislamu na kutambua vipawa vya Qur'ani miongoni mwa Waislamu wa Ulaya. Halikadhalika mashindano hayo yatakuwa fursa kwa wanaharaakti wa Qur'ani kukutana na kubadilishana mawazo. Mashindano hayo yatasimamiwa na majaji wataalamu wa Qur'ani na washindi wanattazamiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwakani.

3617770

captcha