Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, watu
wengine 3,500 wamejeruhiwa, wengi wakiwa na majeraha ya macho, kutokana na
risasi hatari lakini zisizozua zinazutumiwa na jeshi la India kuwakandamiza
waandamanaji.
Mapigano ya sasa yalianza wakati, Burhan Wani ,
kiongozi muandamizi wa chama cha kupigania uhuru wa Kashmir, Hizb ul
Mujahideen, kuuawa akiwa nwa watu wengine wawili baad aya kufyatulaina risasi
na wanajeshi wa India katika eneo la Kokernag mnamo Julai 9.
Mauaji yake yaliibua ghasia kaitka mji wa
Anantanag, ambapo maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakitoa nara za kutaka uhuru.
Wanajeshi wa India wametumia risasi hao, gesi ya kutoa machozi na risasi za
plasitiki zisizoua kuwatawanya waandamanaji.
Mkuu wa Polisi ya India huko Kashmir, K.
Rajendra Kumar amesema kuuawa, Wani ni mafanikio makubwa katika vita dhidi ya
wanamgambo Kashmir. Aidha amejigamaba kuwa polisi wameua wanamgambo 83 huko
Kashmir mwaka huu pekee.
Kashmir ni jimbo lenye Waislamu wengi
India na limekuwa lilikumbwa na mzozo tokea India ipate uhuru kutoka Uingereza
mwaka 1947. Eneo linguine la Kashmir liko Pakistan ambayo pia ilikuwa koloni la
Uingereza. Aghalabu ya Wakaazi wa
Kashmir inayokaliwa na India wanataka kujitenga huku wengine wakitaka kujiunga
na Pakistan. India na Pakistan zimewahi kupigana mara tatu kwa ajili ya Kashmir
ambapo nchi mbili zilitiliana saini mapatano ya usitishwaji via mwaka 2003.
Wakati huo huo Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran imetoa wito kwa utulivu baina ya pande hasimu katika Kashmir
inayodhibitiwa na India. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram
Qassem amesema mzozo wa Kashmir unaweza kutatuliwa kwa njia za Amani na
mazungumzo.
/3460445