Ni qari mwenye talanta ambaye amepata kutambuliwa nchini Algeria. Kwa sasa Sheikh Sahim anaishi katika Umoja wa Falme za Kiarabu na ni Imamu wa sala katika msikiti mmoja huko Ajman.
Mzaliwa wa M’sila, kaskazini mwa Algeria, Sheikh Sahim ameshinda mataji kadhaa katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani.
Ufuatao ni usomaji wake wa Aya 285-286 za Surat Al-Baqarah:
Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako. 285
Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. 286
4194461