Ndege za kivita za Israel siku ya Ijumaa zilishambulia kwa mabomu Msikiti wa Halima katika mji wa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuusawazisha chini.
"Jeshi la Israel lilishambulia kwa bomu Msikiti wa Halima, na kuuharibi kikamilifu," mtu aliyeshuhudia amesema.
Tangu kuanza kwa vita vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba, jeshi la Israel limeharibu kabisa misikiti 88, pamoja na kuharibu kwa sehemu mingine 174. Vikosi vya Israel pia vimlenga makanisa matatu, kulingana na ofisi ya serikali ya vyombo vya habari huko Gaza.
Chini ya sheria za vita, vituo vyote kama hivyo vya kiraia vinapaswa kuwa na mipaka ya kushambulia. Israel imedai kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas linatumia majengo ya raia kama kambi, lakini hadi sasa imeshindwa kutoa ushahidi wowote wa kuridhisha.
3486242