Ee Mwenyezi Mungu! Nitakase nitokamane na taka na uchafu (mwengine), Unipe subira (ili nisubiri) katika mwezi huu juu ya matukio ya Kudira zako, Uniwafikie kwenye kukucha (kukuogopa) na kusuhubiana na wema, kwa msaada wako Ewe Kiburudisho (kitulizo) cha macho ya walio maskini.