Ee Mwenyezi Mungu! Nijaalie katika mwezi huu niwe miongoni mwa wanaoomba maghfira (kwa wingi), pia nijaalie niwe miongoni mwa waja wako wema walio wanyenyekevu, Unijaalie niwe miongoni mwa watu wako walio karibu nawe kwa huruma yako Ewe Mhurumivu wa wanaohurumia.