Tovuti ya al-Kafeel imeripopti kuwa, mpango huo ambao ulianza Alhamisi iliyopita unajumuisha kutembelea maeneo mbali mbali matakatifu nchini Iraq.
Sheikh Saad al-Shimri, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo ya Afrika katika Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS) amesema tayari wanafunzi hao wameshatemeblea haram takatifu za Imam Hadi AS na Imam Askari AS eneo la Samarra na Imam Musa Kadhim AS na Imam Jawad AS huko Kadhimiya.
Mbali na kutekeleza ziara wanafunzi hao pia wamekutana na kufanya mazungumzo na wasimamizi wa maeneo hayo matakatifu.
Al Shimri amesema wanafunzi hao wamekaribisha mpango huo ambao umewapa fursa ya kutembelea maeneo ya kidini katika miji mbali mbali ya Iraq.