Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, mbali na Rais Ebrahim Raisi wa Iran, shakhsia wengine waliohutubu ni pamoja na Ziyad Nakhalah, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina, waziri mkuu wa zamani wa Iraq Adil al-Mahdi, Mufti wa Croatia Aziz Hasanvich, Mkuu wa masuala ya kimataifa wa Harakati ya Hamas Khalil al Hillah, Spika wa bunge la Algeria Bou Abdullah Bou Ghulamullah na wanafikra wengine kadhaa wa Ulimwengu wa Kiislamu.