IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Tishio la Bomu lavuruga Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Washington DC

11:34 - August 19, 2023
Habari ID: 3477462
WASHINGTON, DC (IQNA) - Tishio la bomu lilitolewa dhidi ya Msikiti wa Mohammed (Masjid Muhammad), huko Washington, DC, wakati wa sala ya Ijumaa.

Maafisa wa usalama  eneo hilo walifika msikitini mara baada ya tishio hilo, na kuwaondoa haraka waumini waliokuwa ndani ya msikiti kama hatua ya tahadhari.

Imam Yusuf Selim aliripoti kuwa polisi walifika wakati wa mahubiri baada tishio la bomu. Mohamed Abdulmalik, mkuu wa usalama wa msikiti huo, alitoa wito mara moja kuondoka waumini.

Selim alifafanua kuwa wataalamu wa mabomu walifanya upekuzi katika eneo maalum lililotajwa kwenye tishio hilo. Mara tu ilipodhihirika kwamba tishio hilo halina msingi, umati uliruhusiwa kuingia tena msikitini na kuendelea na Sala ya Ijumaa. Alisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za usalama kwa umakini, haswa katika sehemu ya ibada ya kila siku.

Abdulmalik alibainisha kuwa licha ya kuwa tishio hilo lilikuwa feki, tukio hilo lilirekodiwa rasmi na polisi kuwa ni "uhalifu wa chuki" na hivyo kubainisha haja ya kuendelea kwa mafunzo ya umakini na usalama ili kuhakikisha waumini wanaendelea kuhudhuria msikiti huo katika mazingira salama.

Tukio hilo linakuja huku kukiwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu ambayo Waislamu nchini Marekani wamekumbana nayo, hasa tangu mashambulizi ya 9/11 2011. Kwa mujibu wa uchunguzi wa hivi karibuni wa Taasisi ya Sera na Maelewano ya Kijamii, thuluthi mbili ya Waislamu nchini Marekani waliripoti kukabiliwa na aina fulani ya ubaguzi wa kidini mwaka 2021, na zaidi ya asilimia 90 walisema kuwa chuki dhidi ya Waislamu iliathiri ustawi wao wa kiakili na kisaikolojia Kura ya maoni pia iligundua kuwa Waislamu ndio kundi ambalo lina uwezekano mkubwa wa kukumbwa na uhalifu wa chuki, matamshi ya chuki na unyanyasaji mtandaoni na nje ya mtandao.

3484827

Habari zinazohusiana
captcha