IQNA

Maandamano ya Kuwaunga Mkono Waislamu huko Washington DC

23:36 - July 24, 2016
Habari ID: 3470470
Mamia ya watu, wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu wameandamana Marekani kupinga chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu au Islamophobia..
Katika maandamano hayo yaliyofanyika katika mji wa Washington DC washiriki wamepiga nara kulaani uenezaji wa vitendo vya chuki dhidi ya waislamu na Uislamu. Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamelaani pia vitendo vya kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.

Baadhi ya waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango yenye maandishi na jumbe mbalimbali zinazokemea sera za kueneza chuki dhidi ya Uislamu na kutaka kuionesha dini hiyo mbele ya macho ya walimwengu kwamba, ni tishio kwa amana na usalama wa dunia.

Kaatika taarifa yao waandamanaji hao katika mji mkuu wa Marekani, Washington DC, wamesema kuwa, vitendo vya kundi la kigaidi la Daesh vinapingana na mafundisho sahihi ya dini ya Kiislamu.

Ikumbukwe kuwa, katika majuma ya hivi karibuni vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vimeongezeka mno nchini Marekani na barani Ulaya.

Hivi karibuni Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Ujerumani (ZMD) alisema kuwa, kuna wasiwasi wa kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya bara Ulaya.

Pamoja na kuwepo propaganda chafu dhidi ya Uislamu lakini idadi ya watu wanaosilimu na kuingia katika dini hii tukufu imekuwa ikiongezeka kwa kasi mno katika ulimwengu wa Magharibi.


3517368


captcha