IQNA

Waislamu China

Wajumbe wa OIC watembelea China kukagua hali ya Waislamu mkoani Xinjiang

11:19 - August 18, 2023
Habari ID: 3477454
JEDDAH (IQNA) – Ujumbe wa wawakilishi 25 kutoka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) uliwasili China Alhamisi kujadili uhusiano wa pande mbili na hadhi ya jamii ya Waislamu nchini humo, OIC ilisema katika taarifa yake.

Wajumbe hao wakiongozwa na Balozi wa Djibouti katika OIC Dya-Eddine Bamakhrama walikutana na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Deng Li na maafisa wa Chama cha Kikomunisti cha China. Walibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pamoja, yakiwemo afya na elimu.
Taarifa hiyo pia ilisema kuwa wajumbe hao wanapanga kutembelea Xinjiang, mkoa wa kaskazini-magharibi mwa China ambako Waislamu wengi wa kabila la Uyghur wanaishi. China imekuwa ikishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji dhidi ya Wayghur, lakini Beijing imekanusha madai hayo.
"Ujumbe wa OIC unapanga kuzuru Xinjiang kuangalia hali ya maisha ya jamii ya Waislamu katika eneo hilo," ilisema taarifa hiyo.
OIC ni jumuiya yenye nchi 57 zenye Waislamu wengi, ambayo kwa sasa inaongozwa na Saudi Arabia, ambayo pia ni sehemu ya ujumbe huo. OIC ilisema kuwa ziara hiyo inalenga kuimarisha "ushirikiano wa kimkakati kati ya OIC, nchi wanachama wake na Jamhuri ya Watu wa China."

3484822

captcha