IQNA

China yapiga marufuku sawm ya Ramadhani miongoni mwa Waislamu wa Xinjiang

5:59 - June 19, 2015
Habari ID: 3315931
Serikali ya China imepiga marufuku wanafunzi, walimu na watumishi wa umma katika eneo la Xinjiang lenye Waislamu wengi kutekeleza ibada ya Saumu kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Serikali pia imezuia watu kuhudhuria marasimu yoyote ya kidini ikiwa ni pamoja na ibada za usiku. Taarifa ya serikali imetaka biashara kwenye hoteli na mikahawa kufunguliwa nyakati za mchana kama kawaida. Wanaharakati wa Kiislamu wamepinga agizo hilo la serikali wakisema linalenga kuhujumu dini tukufu ya Kiislamu.

Kwa miaka kadhaa sasa, serikali ya China imekuwa ikitekeleza sheria hiyo ya kibaguzi, na mwaka uliopita, watu kadhaa walifikishwa kortini kwa kukaidi sheria hiyo na kutekeleza ibada ya funga. Ingawa serikali inasema lengo la kuweka sheria hiyo ni kuhakikisha masuala ya dini hayavurugi muundo wa jamii, duru za kuaminika zinasema sheria hiyo ina malengo ya kiuchumi kwani imewekwa ili kuhakikisha nguvu kazi ya taifa haipungui katika mwezi wa Ramadhani.../mh

3315383

captcha