IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya Qur’ani ya Tehran kufunguliwa Jumatatu

17:17 - April 02, 2023
Habari ID: 3476800
TEHRAN (IQNA) – Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ktafunguliwa Jumatatu, Aprili 3, 2023.

Abdolreza Soltani, mkuu wa kitengo cha kimataifa, alisema kuwa kitengo hicho kitazinduliwaa Jumatatu kwa kushirikisha Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Mohammad Mehdi Esmaeili na mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour.

Kitengo hicho kitakuwa na msisitizo maalumu katika suala la umoja wa Kiislamu, alisema, akiongeza kuwa nchi shiriki zitaonyesha kazi za sanaa na kutakuwa na warsha.

Alibainisha kuwa wawakilishi kutoka India, Pakistan, Tunisia, Bosnia, Algeria, Indonesia, Malaysia, Tanzania, Kenya, na Oman wataonyesha kazi zao za sanaa katika maonyesho hayo.

Zaidi ya hayo, baadhi ya nchi zitawasilisha mafanikio yao ya Qur'ani na kuongeza kuwa mataifa hayo ni pamoja na Urusi, Iraq, Algeria, Tunisia, Malaysia, Pakistan, Sri Lanka, Oman, Lebanon na Afghanistan.

Kulingana na Soltani, midahalo ya kielimu pia itafanyika kwa mada tofauti kwa kushirikisha watu kutoka nchi tofauti.

4130940

captcha