IQNA

Umoja wa Waislamu

Afisa Karbala asisitiza Umoja wa Waislamu chini ya Bendera ya Qur'ani Tukufu

19:10 - February 28, 2023
Habari ID: 3476640
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq, amesema Waislamu duniani kote wanapaswa kuungana chini ya bendera ya Qur'ani Tukufu.

Hassan Rashid al-Ajayebi aliyasema hayo katika hafla ya kufunga toleo la 16 la tamasha la kimataifa la ‘Machipuo ya Shahidi’ na kusisitiza pia umuhimu wa kupambana na misimamo mikali na kuendeleza utamaduni wa kuhurumiana.

Alisema moja ya malengo ya tamasha hilo ni kuimarisha utamaduni wa kuhurumiana na kuwasaidia wenye uhitaji.

Alibainisha hayo baada ya wito wa kiongozi mkuu wa Kishia wa Iraq Ayatullah Seyed Ali al-Sistani. Watu wa Iraq na taasisi za kidini walituma maelfu ya tani za msaada kwa walioathirika na matetemeko ya ardhi Uturuki na Syria.

Afisa huyo alirejelea zaidi hitaji la kukabiliana na mikondo potofu na kulinda utambulisho wa kidini na utamaduni.

‘Machipuo ya Shahidi’  au Rabee’-ul-Shahadah  ni hafla ya kitamaduni ya kimataifa ya kidini ambayo hufanyika kila mwaka katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Hussein (AS), Hadhrat Abbas (AS) na Imam Sajjad (AS) katika mwezi wa Sha'aban.

Mwaka huu, hafla hizo tatu ziliangukia Februari 24, 25 na 26 mtawalia.

Hafla hiyo Inalenga kustawisha utamaduni wa Kiislamu na mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS) na kuendeleza mafungamano na Waislamu kote ulimwenguni.

Wajumbe kutoka nchi 44 walishiriki katika hafla hiyo mwaka huu ambapo kulikuwa na vipindi mbalimbali, vikiwemo maonyesho ya vitabu, maonyesho ya sanaa, shughuli za kitamaduni kwa wanawake na duru za Qur'ani vilifanyika wakati wa tamasha hilo, ambalo kauli mbiu yake ilikuwa "Imam Hussein (AS) katika Nyoyo za Mataifa".

 4125045
captcha