Kwa mujibu wa taarifa watu hao waliofikishwa mahakamani mjini Stuttgart Ijumaa wanatuhumiwa kuunda kundi lao linalojulikana kama Group S mwezi Septemba mwaka 2019 ambapo walimiliki silaha kinyume cha sheria.
Imedokwzwa kuwa walkuwa wanapanga kuvuruga amani Ujerumani kwa kushambulia misikiti na kuua au kujeruhiwa Waislamu kwa wingi.
Aidha walipanga kuipindua serikali ya Ujerumani na kutumia mabavu dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa.
Kesi hiyo inaendelea.