IQNA

Adhana yaruhusiwa katika misikiti ya Ujerumani na Uholanzi kusaidia vita dhidi ya corona

21:12 - April 04, 2020
Habari ID: 3472633
TEHRAN (IQNA)- Aidhana ilisikika kupitia vipaza sauti siku ya Ijumaa katika zaidi ya misikiti 100 ya Ujerumani na Uholanzi ikiwa ni hatua iliyotajwa ni ya mshikamano katika vita dhidi ya ugonjwa wa corona.

Kwa mujibu wa taarifa, nchini Ujerumani sauti ya adhana kupitia vipaza sauti ilisikika katika misikiti inayosimamiwa na Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki (DITIB) na Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu (IGMG). Fahrettin Alptekin mwakilishi wa DITIB katika eneo la Essen, Ujerumani amesema kwa kawaida adhana kupitia vipaza sauti hairuhusiwi nchini Ujerumani isipokuwa tu katika nyakati maalumu.

Nchini Uholanzi adhana pia ilisikika katika vipaza sauti vya misikiti ya nchi hiyo ikiwa ni katika mkakati wa mshikamano wa watu wote katika vita dhidi ya corona. Nchini Uholanzi pia kwa kawaida adhana hairuhusiwi kupitia vipaza sauti.

Ujerumani ni nchi ya tatu kwa idadi ya watu walioambukizwa corona barani Ulaya. Hadi kufikia leo, watu 92,150 wameambukizwa corona nchini Ujerumani huku wengine 1,330 wakifariki dunia.

3471040

 

captcha