Kwa mujibu wa
mwandishi wa IQNA, washiriki 98 walishiriki katika mashindano ya kuhifadhi
Qur'ani ambapo kulikuwa na vitengo tafauti vya wanawake na wanaume.
Taarifa zinasema ashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa
ya Kuhifadhi Qur'ani ikishirikiana na Jumuiya ya Kuhifadhi na Kusomesha Qur'ani
Zanzibar.
Washiriki
walishindana katika kuhifadhi Qur'ani Kikamilifu na pia kuhifadhi Juzuu 25, 20, 15, 10, 5 na 3 za Qur'ani
Tukufu.
Aidha Maustadhi wa hadhi ya juu walisimamia zoezi hilo kama
majaji na baada ya hapo washiriki wakapokea zawadi katika sherehe za kufunga
mashindano hayo ambazo pia zilihudhuriwa na maafisa wa serikali na wanazuoni wa
Kiislamu.