IQNA

Kongamano la Fikra za Qur'ani za wanazuoni wa Senegal na Iran

16:54 - October 22, 2016
Habari ID: 3470627
Kongamano la Kwanza la Kuchunguza Fikra za Qur'ani za wasomi wa Iran na Senegal limepangwa kufanyika mwezi ujao wa Novemba katika mji wa Thiès magharibi mwa Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutnao huo ambao utachunguza Fikra za Qur'ani za wasomi wa Iran na Senegal utafanyika kwa ushirikiano na Tariqa ya Ashab Al Yamin nchini Senegal.

Uandalizi wa kongamano hilo umefikiwa katika mkutano baina ya Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Senegal Sayyed Hassan Esmati na Sheikh Mohammad Idriss mkurugenzi wa masuala ya kimataifa wa Tariqa ya Ashab Al-Yamin.

Katika kikao hicho, wawili hao walisisitiza kuhusu udiplomasia wa Qur'ani katika uhusiano wa utamaduni wa Iran na Senegal kwa lengo la kufikia umoja wa umma wa Kiislamu.

Aidha wameafikiana kuwa Kongamano la Kwanza la Kuchunguza Fikra za Qur'ani za wasomi wa Iran na Senegal litachunguza Fikra za Qur'ani za Imam Ruhullah Khomeini RA na Sheikh Amadou Bamba RA ambaye alikuwa maarufu kama Aḥmad ibn Muḥammad ibn Ḥabīb Allāh mwanzilishi wa Tariqa ya Muridiyyah ya Senegal na ambaye aliandika vitabu kuhusu Qur'ani Tukufu.

Pembizoni mwa kongamano hilo la siku moja, kutakuwa na maonyesho ya athari za Qur'ani na filamu za maisha ya wanazuoni hao wawili.

3539680/


captcha