IQNA

Fikra za Kiislamu

Ufahamu wa Ikhlasi katika Uislamu

20:48 - September 29, 2022
Habari ID: 3475856
TEHRAN (IQNA) – Ikhlasi, ni neno linalomaanisha usafi au usafishaji, ni sifa inayokamilisha kila tendo cha watu binafsi na kufikia Ikhlasi kunahitaji kujiboresha.

Kuna marejeleo 50 ya neno "ikhlas" katika Qur'ani Tukufu na inahusu usafi na usafishaji. Wakati kitu kinasemekana kuwa safi, inamaanisha kuwa kitu hicho hakina mchanganyiko wowote wa ziada ndani. Aya ya 66 ya Surat An-Nahl inasema: “Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, vikatoka baina ya baina ya uchafu (matumbo) na damu, maziwa safi mazuri kwa wanywao.” 

Ikhlas inahusiana na mambo ya kiroho na kimaada ya maisha yetu. Kwa hivyo, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Ikhlas na maisha safi au yaliyotakasika. Kuwa na maisha safi ndivyo Qur’ani inavyopendekeza. Hii ina maana kwamba mtu anapaswa kumwabudu Mwenyezi Mungu na kuelekea Kwake kwa ajili Yake tu na hata asiichukulie ibada hii kuwa ni njia ya kwenda Peponi au kuepuka Moto na adhabu.

Umuhimu wa fikra hii unaweza kueleweka kwa namna fulani ikiwa mtu atafikiri kwa kina kuhusu aya ya 51 ya Surah Maryam ambayo inaichukulia Ikhlas kuwa ni miongoni mwa sifa za Mitume wa Mwenyezi Mungu: “Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.”

Shetani alipofukuzwa kutoka mbinguni, aliahidi kuwapoteza watu wote isipokuwa wale ambao hawana lengo lingine isipokuwa Mwenyezi Mungu. “Akasema (Shetani): Naapa kwa Utukufu Wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, isipokuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa.” Qur’ani Tukufu Sura Sa’aad 82-82.

captcha