IQNA

Mwisho Mwema (Khusnul Khatimah)

Mwanamke wa Kiindonesia afariki akiwa anasoma Qur’ani (+Video)

22:34 - September 21, 2022
Habari ID: 3475817
TEHRAN (IQNA) – Video imesambaa mitandaoni inayomuonyesha mwanamke wa Indonesia akianguka wakati akisoma aya za Qur’ani Tukufu.

Video hiyo inayomuonyesha mwanamke huyo akiwa anasoma Qur’ani katika ukumbi imesambaa kwa kasi huku watu wengi wakimuombea dua marehemu.

Video hiyo inaaminika kuwa kutoka kwa mkusanyiko wa kidini ikimuonyesha mwanamke huyo akirudi nyuma polepole huku watu wakikimbia kumuokoa.

Mwanamke huyo aliyekuwa akisoma  aya za Surah Al-Baqara, alihudumiwa haraka na madaktari, na kutangazwa  kufarilki baada ya musa usio mrefu ambapo inaaminika kuwa alipata mshtuko wa moyo..

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamesembaza kilpu, wakimsifu na kusema "amepata mwisho mwema (khusnul khatimah) ambao ni tamanio la kila Muislamu." Pia walimuomba Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.

Matukio kadhaa yaliripotiwa hapo awali ambapo watu walikufa ghafla walipokuwa katika Sala  au wakiwa wanasoma Qur’ani Tukufu.

Tukio kama hilo liliripotiwa mnamo 2018 wakati Muislamu wa Pakistani akiwa Saudi Arabia alianguka wakati akisali.

Mnamo 2017, msomaji wa Qur’ani wa Indonesia alikufa wakati wa usomaji wa Qur’ani katika televisheni. Sheikh Ja’far AbdulRahman alikuwa msomaji anayeheshimika wa Qur’ani wa Indonesia.

Pia mwaka wa 2017, profesa wa chuo kikuu cha Saudi aliaga dunia sekunde chache baada ya kuhitimisha sala ya Alasiri katika msikiti wake.

3480582

captcha