Katika miezi ya hivi karibuni, wasiwasi umeenea ulimwenguni kote kutokana na ukosefu wa chakula, na bei ya ngano na nafaka zingine zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 katika kipindi cha mwezi moja..
Misiri, ambayo ni kati ya watumiaji wakuu wa ngano ulimwenguni, imeathiriwa na uhaba wa bidhaa hiyo na inatafuta njia za kushughulikia hali hiyo.
Akihutubia sherehe ya kuzindua mradi mkubwa wa kilimo Jumamosi, El-Sisi alitaja suala hilo na akasema Misri inakabiliwa na changamoto baada ya kuongezeka kwa bei ya nafaka kutokana na oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine.
Rais wa Misri ameashiria ya 47 ya Surah Yusuf katika Qur’ani Tukufu isemayo: “Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Mtacho vuna kiwacheni katika mashuke yake, isipo kuwa kidogo mtacho kula.”
El-Sisi amewataka Wamisri wafuate mbinu hii ya Nabii Yusuf ambayo ni funzo kuhusu kukabiliana na shida ya chakula na kuongeza usalama wa chakula kwa nchi.
Misiri inahitaji tani milioni 23 za ngano kila mwaka lakini inazalisha tani milioni 9 na hivyo inalazimika kuagiza kutoka nje ili kukidhi mahitaji yake.
4059038