IQNA

Waislamu India

Msomi anaonya kuhusu njama ya kuibua mzozo kati ya Wahindu, Waislamu nchini India

21:44 - May 23, 2022
Habari ID: 3475284
TEHRAN (IQNA)- Mfawidhi Haram Takatifu ya Imam Ridha AS mjini Mashhad anasema umoja kati ya Waislamu na Wahindu ulikuwa muhimu katika kuwashinda wakoloni, na kuongeza kuwa hivi kuna njama za kupanda mbegu za ugomvi kati ya vikundi hivi vya India.

"Umoja na ushirikiano wa Wahindu na Waislamu vimekuwa ufunguo wa mafanikio na nguvu ya India na madola ye kibeberu yanataka kuendeleza  ukoloni kwa kukuza mgawanyiko India," Hujjatul-Islam Ahmad Marvi, mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS, alisema Jumatatu.

Alitoa maoni hayo katika mkutano huko Mashhad na ujumbe wa wasomi wa Kiislamu kutoka India na Bangladesh wakiongozwa na Shahi Imam wa Jamia Masjid huko Delhi Syed Ahmed Bukhari.

Maadui wa Uislamu wakiongozwa na Marekani, Uingereza, na utawala wa Kizayuni wa Israeli daima wamekuwa wakihofia nguvu na umoja wa Waislamu, alisema.

Pia aliita chuki dhid ya Uislamu au Islamophobia kama mkakati mwingine unaotumiwa na maadui kulenga Uislamu na Waislamu. Mabeberu walounda kundi la kigaidi la Daesh (ISIS au ISIL) ili kutekeleza mauaji ya Waislamu na kuarifisha Uislamu kama dini ya vurugu, alisema.

Kwa upande wake, Syed Ahmed Bukhari alisifu usimamizi mzuri wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS licha ya idadi kubwa ya wafanyaziara.

"Kusudio la safari yetu Iran ni kukutana na wasomi wa Kiislamu na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Waislamu wa Iran na India," ameongeza.

Ujumbe huo ulikutana na mfawidhi wa Haram ya Hazrat Masoumeh (SA) katika mji wa  Qom Ayatullah Seyyed Mohammad Saeidi Alhamisi.

5496866

captcha