IQNA

Askari wa Israel wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kuwajeruhi Wapalestina

16:05 - February 20, 2019
Habari ID: 3471847
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel Jumanne waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) na kuwajeruhi Wapalestina waliokuwa wakifanya ibada katika eneo hilo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu.

Taarifa zinasema Wapalestina wasiopungua 10 walijeruhiwa Ijumaa jioni baada ya askari wa utawala wa Israel kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa kupitia mlango wa Bab al Rahma.

Aidha katika tukio hilo la kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu, wanajeshi wa Isreli waliwakamata Wapalestina 15 ambapo aghalabu ya waliokamatwa ni wanafunzi wa chuo cha kidini.

Siku ya Jumatatu, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walikuwa wameufunga mlango wa Bab al Rahman a kuwazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa.

Utawala haramu wa Israel unauvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa katika hali ambayo watawala wa nchi za Kiarabu wakiongozwa na Saudi Arabia wana uhusiano wa siri na Israel na wako mbioni kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo unaokalia kwa mabavu qibla cha kwanza cha Waislamu na ardhi za jadi za Wapalestina.

3467968

captcha