IQNA

Kongamano la Miujiza ya Qur'ani Lafanyika Baghdad

13:25 - February 18, 2019
Habari ID: 3471845
TEHRAN (IQNA)-Kongamano la kimataifa la miujiza ya Qur'ani Tukufu limefanyika hivi karibuni katika mji mkuu wa Iraq, Baghadad.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limehudhuriwa na wanazuoni na wasomi wa Qur'ani kutoka nchi mbali mbali duniani.

Kauli mbiu ya kongamano hilo ilikuwa ni "Dhihirisho la Qur'ani Katika Zama za Sayansi".

Kati ya wageni wa heshima katika kongamano hilo alikuwa  Mufti wa Quds (Jerusalem) Sheikh Akrama Sabri, mwakilishi wa Al Azhar Sheikh Mohammad Wassam, mwanazuoni mashuhuri wa Qur'ani Sheikh Zaqul Najjar na ujumbe wa ngazi za juu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO. Kati ya mada zilizojadiliwa ni taalaum za tiba, kosmolojia na jiolojia.

Kongamano hilo liliandaliwa na Idara ya Wakfu wa Masunni Iraq na lilifanyika katika ukumbi wa Msikiti wa Umul Quraa mjini Baghdad.

3790968

captcha