IQNA

Waislamu 90 Marekani wanawania viti vya uongozi

15:02 - August 07, 2018
Habari ID: 3471621
TEHRAN (IQNA)- Waislamu zaidiya 90 nchini Marekani wanawania nafasi mbali mbali za uongozi katika ngazi za mitaa, jimbo na kitaifa mwaka huu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa na taasisi ya kiraia ya Jetpach inayowatetea watu wa jamii za waliowachache, aghalabu ya Waislamu wanawania nafasi za uongozi ni wafuasi wa chama cha Democrats. Taasisi hiyo imesema idadi hiyo mwaka huu ni kubwa Zaidi ya wakati wowote ule tokea hujuma za Septemba 11 mwaka 2001 ambazo zilipelekea Waislamu Marekani wakumbane na kila aina ya ybaguzi na ukandamizaji.

Bi. Deedra Abboud, mgombea wa kiti cha Baraza la Senate kutoka jimbo la Arizona kwa tikiti ya chama cha Democrat anasema ameamua kuingia katika siasa baada ya Donald Trump kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Abboud ambaye ni wakili na mtetezi wa haki za binadamu anasema miaka 15 iliyopita mjadala miongoni mwa Waislamu Wamarekani ulikuwa ni kuhusu iwapo wanapaswa kushiriki katika uchaguzi. Anasema baada ya 9/11 Waislamu walikumbwa na wimbi kubwa la chuki dhidi ya Uislamu lakini anaongeza kuwa hali hivi sasa ni mbaya Zaidi baada ya kuchaguliwa Trump.

Weledi wa mambo wanasema chuki zinazoenezwa na Trump ndizo ambazo zimetoa motihsa kwa Waislamu Wamarekani kuwania viti katika nafasi za uongozi ili kuelimisha jamii kuhusu Uislamu na Waislamu.

3466496

captcha