IQNA

Mashindano ya Qur'ani kwa waliosilimu Abu Dhabi

21:16 - May 15, 2018
Habari ID: 3471514
TEHRAN (IQNA)- Taasisi katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeandaa mashindano ya Tarteel ya Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani maalumu kwa waliosilimu.

Mashindano ya Qur'ani kwa waliosilimu Abu DhabiKituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Nyumba ya Zayed (ZHIC) katika mji mkuu wa UAE, Abu Dhabi, kimetangaza hafla kadhaa maalumu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani maalumu kwa waliosilimu ikiwa ni pamoja na vikao vya mashindano ya kusoma Qur'ani Tukufu na mihadhara ya kidini kuhusu sawm na futari.

Washiriki watapata mafunzo kuhusu saumi kwa lugha mbali mbali pamoja na mafunzo ya Uislamu kwa ujumla.

Aidha kutakuwa pia na maonyesho ya Sanaa za Kiislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yatakayojumuisha kaligrafia ya Qur'ani Tukufu.

Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Nyumba ya Zayed kimetangaza kuwa lengo kuu la kuandaa mashindano ya Tarteel ni kustawisha maarifa ya Qur'ani miongoni mwa waliosilimu.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Alhamisi tarehe 17 Mei katika aghalabu ya maeneo ya dunia.

3465845

captcha