IQNA

Madrassah 14,000 za Qur'ani Yemen zina wanafunzi 450,000

17:20 - December 04, 2017
Habari ID: 3471294
TEHRAN (IQNA)-Kuna madrassah za Qur'ani zipatazo 14,000 nchini Morocco ambazo zinatoa mafunzo ya Qur'ani kwa wanafunzi 450,000 ambapo asilimia 40 kati yao ni wanawake.

Akizungumza kwa munasaba wa sherehe za Maulidi ya Mtume SAW, Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu Morocco Ahmed Toufiq amesema madrassah za Qur'ani zina nafasi muhimu nchini humo. Aidha amesema leseni mpya zimetolewa kwa ajili ya kuanzisha madrassah zingine 300 mpya za Qur'ani ambazo zitapewa himaya na serikali na kwamba idadi kubwa ya madrassha za Qurani zimekarabatiwa.

Katika misikiti yote Morocco, kuna ukumbi ulio kando ya kila msikiti ambao hutumiwa kuwafundisha Qur'ani Tukufu watoto kuanzia umri wa miaka mitano. Aidha watoto watoto hapo hujifunza lugha ya Kiarabu, kaligrafia na taaluma zinginezo.

Wanafunzi wanaofuzu katika wanaingia katika awamu ya pili katika madrassah ambazo nchini humo ni maarufu kama zawia. Katika nchi mbali mbali za Kiislamu duniani madrassha za Qur'ani huwa na majina maalumu. Kwa mfano nchini Libya hujulikana pia kama zawia, Somalia ni maarufu kama dox, Senegal hutiwa daara,  Misri ni kuttab na Mauritania ni mahadra huku katika maeneo mengine majina kama vile maktab au madrassah yakitumika.

captcha